PSG WALIMTAKA NEYMAR KWA EURO 190 MILLION

Wagner Ribeiro.,mmoja wa wawakilishi wa Neymar, amedai Paris Saint-Germain walikuwa tayari kutumia € 190million toka Barcelona katika dirisha la usajiri lililopita.

PSG walitaka kumpa Neymar mkataba ambao ungemwezesha kuvuna
€767,000 (£650,000) kwa wiki,kwa mjibu wa Ribeiro,lakini Barcelona waliikataa ofa hiyo na badala yake wakamshawishi Neymar kusaini mkataba mpya wa miaka 5.

"Alikuwa karibu sana na kujiunga na PSG.  angeweza kupokea € 40m kwa mwaka [baada ya kodi]. PSG walikuwa tayari kulipa  € 190m."alisema Wagner Ribeiro.

"Neymar alikuwa pia karibu  kuhamia Manchester United. Lakini akachagua kusaini  mkataba mpya na   Barcelona kwa fedha pungufu, ​​kwa sababu alitaka kubaki katika Barcelona."

Lakini PSG walikanusha madai ya Ribeiro,wakisema ni uongo mtupu.